The Hijri Calendar Converter Widget
requires Adobe Flash
Player 7 or higher.

To view it, click here
to get the latest
Adobe Flash Player.
Yaliyomo
Nyumbani
Quraan
Ukumbi
Makala
Fiqh
Sira
Maadili
Itikadi
Habari
Videos
Mapishi
Mawaidha
Ratiba Ya Swalah
Vitabu
Quiz
Matangazo
Fomu
Hadiyth 40
Hadiyth Za Wiki
This Month Newsletter
HABARI
Nyumbani arrow Habari arrow Latest arrow Ujumbe wa Ramadhaan
Ujumbe wa Ramadhaan PDF Print E-mail
Saturday, 15 August 2009

Assalaam Alaykum

  Allah Subhaanahu Waa’ala Anasema katika Qur’aan tukufu:

“Enyi Mlioamini mmeandikiwa Saumu Kama Walivyoandikiwa Waliokuwa Kabla yenu ili Mpate Kumcha MwenyeziMungu” Qur’an 2:183

InshaAllah panapo uzima mwezi mtukufu wa Ramadhani utaanza tarehe 20-21/08/09, na kama kawaida yetu tutakuwa tunakutana kila siku ya Jumamosi katika Hall la Kingsheath kuanzia saa kumi kamili jioni mpaka saa Nne na nusu usiku, kwa ajili ya Darsa, Futari na Swalah kwa wale watakaojaaliwa.

Jumuiya yako ya Al Iman kwa Ramadhaan hii inshaAllah imejipanga katika programu itakayokuletea kwa muda wa takriban wiki sita mfululizo kuanzia Jumamosi ya tarehe 15/08/2009 ambapo tutamkaribisha Ustaadh Faysal kutoka Leicester katika Mada yake muhimu ya jinsi ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhaan.

Jumamosi itakayofuatia ya tarehe 22/08/09 ambayo inawezekana ikawa ndiyo Ramadhaan ya kwanza au tarehe 30 Shaaban. Kwa siku hii program yetu itaanza saa 12.00 jioni badala ya saa kumi jioni kwa sababu ndio muda tuliofanikiwa kuupata ukumbi. Siku hii tutakuwa pamoja na Ustaadh Abdurrazzaaq katika kujiandalia program yetu ya Ramadhaan ya mwaka huu inshaAllah.

Program za siku zitakazofuatia mtajuulishwa InshaAllah.

Ili kufanikisha shughuli hii InshaAllah tunaomba ushirikiano wa waumini wote kwa hali na mali, na yafuatayo yanahitajika;

  • Mahudhurio yenu kwa wingi.

  • Michango ya hali na Mali.

Lengo la kukutana ni kukumbushana mambo ya kheri hasa katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhaan na kufutari pamoja. Tujitahidi kufika mapema na kwa wingi, watakaojaaliwa kutoa sadaka zao wanakaribishwa kwa njia yeyote ile.

Mtume Muhammad (Swallah Llahu Alayhi Wa-alihi Wasallam) anasema katika hadith sahihi:

“Mtu ambaye atamfuturisha aliyefunga atapata ujira mfano wa yule aliyefunga pasina kupungua chochote ktika ujira wa mfungaji mwenyewe”

Ni fadhila kubwa kwa yule aliyefunga na akamfuturisha mtu mwingine aliyefunga. Tunamuomba Allah (Subhaanahu Wattaallah) azikubali Swaumu zetu inshaallah.

Kwa maelezo zaidi na kama unataka kuchangia kwa chochote unaweza kuwasiliana na wafuatao:-

Ameer – Ustaadh Abdurrazzaq   – 07951 816 208

Naibu Ameer –Ustaadh  Ja’afar – 07971 809 927

Ukhti Kadhya- 07950 442 711

Wabillahi atTawfiyq

         
Last Updated ( Friday, 16 October 2009 )
 
< Prev   Next >
Administrator
Wahusika

 

© 2010 Madrasatul Iman al – Islamiyyah

Web Master