The Hijri Calendar Converter Widget
requires Adobe Flash
Player 7 or higher.

To view it, click here
to get the latest
Adobe Flash Player.
Yaliyomo
Nyumbani
Quraan
Ukumbi
Makala
Fiqh
Sira
Maadili
Itikadi
Habari
Videos
Mapishi
Mawaidha
Ratiba Ya Swalah
Vitabu
Quiz
Matangazo
Fomu
Hadiyth 40
Hadiyth Za Wiki
This Month Newsletter
HABARI
Nyumbani arrow Habari arrow Latest arrow Update Kuhusu Kitengo cha Misiba
Update Kuhusu Kitengo cha Misiba PDF Print E-mail
Sunday, 06 September 2009

Assalaam Alaykum.

Kutokana na kumbukumbuku zetu inaonesha bado  ada za kuchangia mfuko wa Misiba hazitolewi kwa wakati na baadhi yetu tumejisahau kabisa.

Kuna wachangiaji ambao wana malimbilikizo kutokea 2007 na kwa maana hii ni kuwa hata 2009 bado hali ya uchangiaji si ya kuridhisha hata kidogo.

Tulikuwa na utaratibu wa kuandikiana kwa madhumuni kukumbushana kila baada ya muda kuhusu uchangiaji lakini kwa bahati mbaya haukufanya kazi na baadae kitengo kikaamuwa  kuondoa ule utaratibu wa kumfuta mchangiaji mwenye malimbikizo lakini pia matunda yake sio ya kuridhisha.

Kupunguwa kwa gharama za mazishi  kutokana na  mabadiliko ya mfumo wa mazishi yetu ( kuzika bila ya kupitia kwa Mkurugenzi wa Mazishi), kitengo cha Misiba  kinafikiria kutowa ubani kwa wachangiaji ambao wana familia zao nyumbani ikiwa ni baba na mama mzazi, mke na mtoto wa kumzaa.Kiwango kitaamuliwa baada ya kupitishwa na ngazi zote za Jumuiya.

Watakaofaidika na ubani huu ni wale ambao watakaokuwa wamelipia ada zao bila ya kuwa na malimbikizo yasiyozidi miezi mitatu.

Kama ni miongoni mwa walio na malimbikizo jitahidi kulipa mapema na tunakushauri  kutumia njia ya Standing order ambayo itakusaidia sana kuondokana na usumbufu huu.

Kitengo kinawatakia Ramadhaan njema na Insha Allah Moja atukubalie funga zetu na ibada zetu zote katika mwezi huu na iwe ni Darsa kwa miezi yote katika maisha yetu Amin.

Wabillah Tawfiyq.

Last Updated ( Friday, 16 October 2009 )
 
< Prev   Next >
Administrator
Wahusika

 

© 2010 Madrasatul Iman al – Islamiyyah

Web Master