The Hijri Calendar Converter Widget
requires Adobe Flash
Player 7 or higher.

To view it, click here
to get the latest
Adobe Flash Player.
Yaliyomo
Nyumbani
Quraan
Ukumbi
Makala
Fiqh
Sira
Maadili
Itikadi
Habari
Videos
Mapishi
Mawaidha
Ratiba Ya Swalah
Vitabu
Quiz
Matangazo
Fomu
Hadiyth 40
Hadiyth Za Wiki
This Month Newsletter
HABARI
Nyumbani
HII NDIO ITIKADI SAHIHI YA KIISLAM (SEHEMU YA KWANZA) 1
Wednesday, 27 January 2010

 Shaykh Muhammad Bin 'Uthaymiyn
Imetarjamiwa Na Muhammad Faraj

Shukrani zote ni zake Mola wa uliwengu wote, na mwisho mwema ni wa wamchao Mwenyezi Mungu, na hapana uadui isipokuwa kwa madhalimu.

 

Nashuhudia kuwa hapana anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah Peke yake asiye na mshirika mwenye Ufalme na haki iliyo wazi, na nashuhudia kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mjumbe wake na Mtume wake na mwisho wa wajumbe wake, na ni kiongozi wa wacha Mungu. Mola wetu msalie na msalimie Mtume wako huyu pamoja na Masahaba wake na kila atakayemfuata kwa wema na uongofu mpaka Siku ya Qiyaamah.

 

Amma baad,

Hakika Mwenyezi Mungu amemtuma Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) awe dalili iliyo wazi  juu ya waja wake wote, na awabainishie yale aliyoteremshiwa katika kitabu, na awe mfano mwema wa kuigwa na walimwengu wote, na ili watu wapate kuwa na muongozo mwema katika dini yao na dunia yao.

 

Last Updated ( Wednesday, 27 January 2010 )
Read more...
 
Namba mpya kwa ajili ya Madrasah
Sunday, 17 January 2010

Assalaam Alaykum

Tunapenda kuwataarifu Wazazi pamoja na wanafunzi kwamba endapo mwanafunzi atakosa kuhudhuria Madrasah atapaswa kuifahamisha Madrasah haraka iwezekanavyo.

Kuanzia tarehe 20/01/2010 Namba mpya ya Madrasah kwa wenye udhuru wa aina yoyote ni 07961 284 919.

Namba hii itatumika kwa njia ya simu au kutuma ujumbe wa sms. Kuanzia sasa Wazazi hawatotakiwa kutumia simu za Walimu bali watapaswa kutumia nambi hii mpya.

Kutoijulisha Madrasah kwamba mwanafunzi hatohudhuria kunaweza kupelekea hatua za kinidhamu kuchukuliwa kwa mujibu wa muongozo wa Madrasah

Wajazaakumu Llaahu Khayraa

 
UZURI WA KUSALI SALA ZA SUNNAH (ZILIZOSISITIZWA)
Saturday, 16 January 2010

Kutoka kwa mama wa waumini Ummu Habiybah, radhi za Allaah ziwe juu yake amesema; Nimemsikia Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallam akisema;  

Mja yeyote Muislamu anayeswali kwa ajili ya Allaah – kila siku rakaa kumi na mbili za kujitolea (Sunnah) ambazo sio za fardhi, Allaah Atamjengea nyumba peponi. [Muslim].

Maelezo:

Hadithi hii inahimiza na kuonyesha umuhimu wa Sala za Sunnah zilizokokotezwa, ambazo husaliwa kabla/baada ya Sala za fardhi.  Malipo yake ni kujengewa nyumba kwenye pepo kwa mwenye kuzitekeleza. 

Sala hizi ni kama ifuatavyo.

Rakaa mbili kabla ya Sala ya Alfajiri

Rakaa nne (mbili mbili au kwa pamoja*) kabla ya Sala ya Adhuhuri

Rakaa mbili baada ya Adhuhuri

Rakaa mbili baada ya Sala Magharibi

Rakaa mbili baada ya Sala ya ‘Ishaa 

Pia kuna Hadithi nyengine ya Mtume Swalla Llaahu ‘Alayhi Wasallam iliyopokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim ambayo inasema ni rakaa kumi ambazo ni sawa hizi ila kwa Adhuhuri huwa ni rakaa mbili tu kabla.

·         Kutokana na baadhi ya mapokezi inakubalika kusali rakaa nne za kabla ya Adhuhuri kwa pamoja zote na kwa Tashahhud moja tu na kisha kutoa Salaam. Na kuziswali rakaa mbili mbili ni bora zaidi; kila rakaa mbili unakaa Tashahhud na kutoa salaam ni bora zaidi kuliko kuziswali zote nne pamoja japo inaruhusiwa.

Last Updated ( Saturday, 16 January 2010 )
 
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>

Results 17 - 20 of 84
Administrator
Wahusika
Aya za Quran
Displaying:
Srh. Al-Baqarah (2)
Ayat 87
 Listen to this ayat (verse) 
2.87 . Na hakika tulimpa Musa Kitabu na Tukawafuatisha Mitume (wengine) baada yake. Na tukampa Isa, mwana wa Maryam, hoja zilizo wazi na tukamtia nguvu kwa roho mtakatifu (Jibriyl). Basi walipokufikieni Mitume kwa yale yasiyoyapenda nafsi zenu, mlijivuna, kundi moja mkalikadhibisha na kundi (jengine) mkaliua.

[ Srh. Al-Baqarah : 87 ]
Who's Online
We have 1 guest online

 

© 2010 Madrasatul Iman al – Islamiyyah

Web Master