|
KUWA NA HAMU YA MALI NA ELIMU NA KUITUMIA KWA AJILI YA ALLAH |
|
Friday, 04 December 2009 |
Kutoka kwa Abdullah Ibn Mas`ud, radhi za Allah ziwe juu yake: Mtume Swalla Llahu ‘Alayhi Wassalam amesema:"Hakuna husda (wivu) ila kwa mambo mawili: mtu aliejaaliwa mali na akaitumia kwa njia nzuri, na kwa mtu aliejaaliwa elimu na kuifanyia kazi na kuwafundisha wengine.” [Al-Bukhari na Muslim]
Maelezo: Hadithi inatilia mkazo kujifunza elimu yenye manufaa pamoja na kutumia mali kwa ajili ya Allah Subhaanahu Wata’ala. Elimu bora ni ile inayotokana na Quraan pamoja na Sunnah. Muislamu amekatazwa kumhusudu mwenziwe. Husda imeruhusika pale tu mtu anapomuona mwenziwe amejaaliwa uwezo wa mali na elimu na akazishukuru neema hizo kwa kuzitumia kwa ajili ya Allah Subhaanahu Wata’ala. Hapo ndipo unaweza kumuonea wivu mtu kama huyo kwa kutumia alivyobarikiwa na Mola wake kwa njia nzuri zitakazomridhisha Allah Subhaanahu Wata’ala. |
|
|
Njia ya Watu Wema Waliotutangulia |
|
Sunday, 01 November 2009 |
|
Muhaadhara uliofanyika Northampton tarehe 12 Dhul Qaidah 1430- 31/10/09.Ni Muhaadhara ambao Ustaadh Badru Ja’far alituandalia kwa kutuaga baada ya kumaliza shughuli iliyomleta hapa Uingereza ya masomo na kutuusia tushikamane na njia za waja wema waliotutangulia. |
|
|
Sunday, 01 November 2009 |
ABU ‘AMMAAR3 NIFASI Nifasi kilugha ni kujifungua. Mwanamke aliyejifungua kwa lugha ya kiarabu huitwa Nufasaa.Ama Nifasi kisheria ni Ni damu anayotoka mwanamke kabla, wakati wa kujifungua na kuendelea kutoka kwa muda maalum.Damu ya Nifasi inaweza kutoka kabla ya kujifungua ambapo baadhi ya wanawake wanapovunja chupa kwa mfano wanaweza kuona damu. Hivyo ikitoka kabla ya kujifungua na wakati chupa imekwishapasuka itahesabika ni Nifasi. Pia huendelea kwa muda mpaka itakapokatika. Damu inayotoka ni baada ya kujifungua ambapo fuko la uzazi hujisafisha |
|
Last Updated ( Sunday, 01 November 2009 )
|
|
Read more...
|
|
|
|
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>
|
| Results 25 - 28 of 84 |