|
IYDULFITWRY KATIKA KIWANJA CHA KINGSHEATH-NORTHAMPTON TAREHE 20/09/2009. 1 SHAWAAL-1430H (ABU ABDIRAHMAN) NAMSHUKURU ALLAH SUBHANAHU WATAALA YEYE PEKEE NDIYE APASAYE KUABUDIWA, NA SWALA NA SALAMU ZIMFIKIYE ALHABIB MUSTWAFAA SWALLA LLHAHU ALAYHI WASALLAM. Tunahuzunika na kusikitika na kuliya kwa kuondokewa na mgeni mtukufu mwezi wa Ramadhani, mgeni ambaye alikuwa nasi akiwa amebeba kila aina za kheri katika amali njema, ama hakika zina furaha nafsi za wale waliofaidika na kuneemeka na kheri za mgeni huyu. في حديث ابن عباس المرفوع لله في كل ليلة من شهر رمضان عند الإفطار ألف ألف عتيق من النار، كلهم قد استوجبوا النار، فإذا كان آخر ليلة من شهر رمضان أعتق الله في ذلك اليوم بعدد ما أعتق من أول الشهر إلى آخره Imepokewa hadithi na Ibni Abbas Radhi za Allah zimfikiye, mtume Swalla llahu alayhi wasallam kasema: Allah Subhanahu wataala katika kila usiku wa mwezi wa Ramadhani wakati wa kufuturu huwaacha huru maelfu kwa maelfu katika watu wa motoni, wote wakiwa wakistahiki kuingia motoni, na unapofika usiku wa mwisho huwaacha huru kwa jumla ya idadi kama ile ya mwanzo wa mwezi mpaka mwisho wake. |