English Site | New Swahili Site
Home Mapishi Mchuzi wa Pweza
Mchuzi wa Pweza PDF Print E-mail
Monday, 28 December 2009 08:53

Sample Image

 

Vinavyohitajika

·         Pweza 1

·         Chumvi

·         Ndimu 1 kubwa na yenye maji ya kutosha

·         Kotmiri kidogo

·         Bizari ya manjano

·         Nazi nusu (cream coconut)

·         Tungule kibati 1 au zikiwa fresh 3 za kiasi

·         Tomato puree vijiko 2 vya chakula

·         Kitunguu maji 1 kikubwa

·         Thomu na tangawizi ya kusagwa

·         Mafuta ya kupikia vijiko 4 vya chakula

Namna ya kutayarisha na kupika

·         Msafishe  Pweza  vizuri na umkatekate vipande upendavyo

·         Muweke kwenye sufuria na umtie thomu na tangawizi iliyosagwa kijiko 1 cha chai, umuwache awive kwa maji yake mwenyewe (usimtie maji  wala chumvi)

·         Saga nazi yako kwa kipimo cha maji magi 1

·         Akishawiva pweza, muweke kando

·         Injika sufuria yenye mafuta, katakata kitunguu na kutia kwenye sufuria  yenye mafuta na uanze kukikaanga.

·        Kikishapiga wekundu wa zafarani, weka kijiko kimoja cha thomu na tangawizi iliyosagwa  pamoja tungule na kisha ukaange vizuri.

·        Zikishawiva ,weka tomato puree vijiko 2 vya chakula na usubiri viwive vizuri kwa muda wa dakika 2.

·         Kamua ndimu na uweke katika mchuzi, koroga kidogo

·         Na tayari wakati wakati wa kuweka tui la nazi yako uliyokwisha ichuja na kuisaga vizuri.

·         Koroga kidogo na uonje chumvi na kama haijaridhisha ladha yake ongeza kidogo.

·        Katakata majani ya kotmiri ndani ya mchuzi pamoja na pweza  subiri kwa dakika 1 uchemke  kisha pakuwa na tayari kwa kuliwa.

Kidokezo

Unapomchemsha pweza,  usiweke chumvi kwani mara nyingi anakuwa na chumvi yake mwenyewe.

 

 

Administrator

Wahusika